Viatu vya Ngassa vigumu kurithi
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga aliyesajiliwa kutokea
Mbeya City, Deus Kaseke amekiri wazi kuwa viatu vya Mrisho Ngassa ni vizito mno
kurithi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya
kutambulishwa rasmi na Yanga katika mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani, Kariakoo
Dar es salaam, Kaseke alisema atapambana kuziba pengo la Ngassa ambaye siku za
karibuni ametimkia Free State Stars ya Afrika kusini akiwa mchezaji huru.
Kaseke akitambulishwa rasmi jana
“Namheshimu sana Mrisho Ngassa kwa jinsi anavyocheza na staili
yake, kuvaa kiatu cha Ngassa au kucheza kwa staili yake ni vigumu, lakini
nitapigana mwanzo mwisho ili niweze kuziba pengo lake”. Amesema Kaseke na
kusisitiza: “Niwaambia kitu kimoja, nimetoka Mbeya City kuja hapa Yanga kwa lengo
la kufanya kazi, nitajituma zaidi, nilipoishia nitaongeza ili mwalimu aweze kunipa nafasi, sina mambo mengi naomba
Mungu aniongeze katika hili”.
Kaseke ambaye ni pendekezo la kocha wa Yanga, Hans van der
Pluijm pia amesema kujiunga Yanga ni nafasi kwake kuitwa timu ya taifa.
“Jinsi tulivyozoea, timu ya taifa hawaangalii sana timu za
mikoani, naona nikifanya vizuri hapa Yanga, nitapata nafasi timu ya taifa”.
Ameeleza Kaseke.
0 comments:
Post a Comment