Mpira wa bara la Ulaya utakuwa na mabadiliko makubwa sana kama ikitokea Lionel Messi anaondoka Barcelona, hii ni kauliya kocha wa Chelsea Jose Mourinho.
Messi amekuwa ni mtu muhimu sana katika klabu ya Barcelona kwa takribani muongo mmoja sasa, akiwasaidia kutwaa makombe matatu ya ligi ya mabingwa Ulaya, makombe sita ya La Liga na mengine kadhaa ambayo hayajatajwa.
Mourinho, ambaye alimpoka taji la La Liga Guardiola mwaka 2012 wakati akiinoa Real Madrid anahisi kuwa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 27 ndio nguzo kubwa ya mafanikio ya klabu hiyo
"Ndani ya kipindi cha miaka 10 ambacho Messi hatokuwepo, ramani ya soka la Ulaya lazima itabadilika sana," Mourinho aliiambia talkSPORT.
"Walichoshinda Barcelona katika miaka kadhaa iliyopita wakiwa ama na Frank Rijkaard, Pep Guardiola au Luis Enrique kama makocha ni kwa sababu wamekuwa na kiumbe huyu."
Chelsea wamewahi kuhusishwa na kumwania Messi, ambaye kwa wakati fulani alionekana kutokuwa na furaha klabuni hapo, lakini Mourinho alikanusha vikali taarifa hizo.
0 comments:
Post a Comment