KATIBU Mkuu wa Simba, Stephene Ally, ametangaza kujiuzulu
nafasi hiyo baada ya madaktari wa timu ya taifa ya Muhimbili kumshauri kupumzika
kwa muda usiojulikana kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo.
Stephene aliingia madarakani mwaka jana
mara baada ya uongozi kuingia madarakani kuiongoza timu hiyo chini ya Rais
Evans Aveva.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na kukaririwa na Salehjembe, Stephene amesema kikubwa
kilichomfanya ajiuzulu ni kutokana na matatizo ya kiafya.
“Cha kwanza kabisa katika mwili wa binadamu ni afya na hayo
mengine yanakuja baadaye, madaktari wamenishauri nipumzike kufanya kazi kwa
muda usiojulikana kwa ajili ya kujiuguza kwanza. Ugonjwa sitaweza kuutaja kwa
sasa, tayari nimekabidhi barua kwa uongozi.
“Ninaomba nichukue muda huu kuwashukuru viongozi, wachezaji
na mashabiki kwa jumla kwa kipindi chote nilichokuwa ninaiongoza Simba,”
alisema Stephene.
0 comments:
Post a Comment