Julio kamwe! hawezi kuifundisha Yanga
KOCHA mwenye maneno mengi, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’
amethibitisha kuwa kamwe hawezi kuifundisha klabu ya Yanga katika maisha yake ya
kufundisha mpira wa miguu.
Julio alikuwa anaiambia E-fm usiku huu kwamba katika maisha
ya mpira leo unaweza kuwa klabu hii kesho nyingine, wakati anataja klabu
mbalimbali akaitaja Yanga, ghafla alifuta kauli yake kwa haraka akidai hawezi
kuifundisha Yanga.
“Katika mambo ya mpira kuna leo na kesho, leo nipo Mwadui,
kesho nipo Coastal, keshokutwa nitakuwa Yanga, aaah! Yanga hapana, keshokutwa
nitakuwa Simba, hayo ndio maisha ya mpira”. Amesema Julio na kusisitiza: “Unajua
Yanga ni timu ambayo wao wenyewe hawaniamini, lakini kwa utaratibu wa kimpira
unaangalia wapi kwenye maslahi. Kama kocha natakiwa kuwa kocha wa timu yoyote inayonihitaji, kama hivi
nilikuwa Simba, nikaenda Mwadui, nimekuwa Coastal, kesho inatakiwa niwe Mbeya
City, lakini kwa huu utamaduni wetu wa Kitanzania kwamba wewe ukiwa kocha wa
Simba basi uwe umecheza Simba na uwe kocha wa Simba tu, hutakiwi kwenda klabu
nyingine si mzuri, leo hii Fred Minziro au Charles Boniface hawezi kuifundisha
Simba, sasa hii si maana halisi ya ukocha.
0 comments:
Post a Comment