KOCHA aliyeipandisha daraja Mwadui fc na kwenda kuinusuru
Coastal Union kushuka daraja msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amekiri kuwa ana asilimia kubwa ya kubaki kwa matajiri
wa madini wa Mkoani Shinyanga baada ya kufanya mazungumzo ya maana.
Julio amesema kwa takribani asilimia 99 amemalizana na
Mwadui ambako atasaini mkataba wa miaka mitatu, lakini ameitwa na Coastal Union,
hivyo anakwenda kuwasikiliza kesho jijini Tanga.
“Juzi nimetoka zangu Mwadui kufanya nao mazungumzo, kuna
mambo mengi mazuri tumeongea nao kwa takribani asilimia 99. Coastal nao
wameniita, naenda kuwasikiliza ni kitu gani wataniambia, baada ya hapo
nitaongea kiundani ni wapi nimesimamia, lakini inavyoonekana nina nafasi kubwa
ya kubaki Mwadui”. Julio ameiambia E-fm
na kuongeza: “Mimi nitasema kile ambacho nimeongea na Mwadui, kibinadamu sio vizuri
wenzio wanakuita, halafu unakataa kwa kujiona kama wewe ndio bora kuliko watu
wote. Nakwenda kuongea nao kibinadamu, naenda kuwashukuru kwasababu nimefanya
nao kazi salama”.
0 comments:
Post a Comment