·
John Terry alicheza kila dakika wakati
Chelsea ikiweza kunyakua taji la Ligi Kuu
·
Terry anaungana na mlinzi wa zamani,
Gary Pallister
·
Gary Pallister, Mlinzi wa zamani wa
Manchester United, alifanya hivyo msimu wa 1992-93
·
Mafanikio haya ya Terry, yamekuwa ni
dhihaka kwa bosi wake wa zamani, Rafa
Benitez
Nahodha wa Chelsea, John Terry amekuwa mchezaji wa
pili wa ndani (mchezaji ambaye sio kipa) kuweza kucheza kila dakika katika
kampeni ya timu yake kushinda Ligi Kuu ya Uingereza.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya
Uingereza, amekuwa mchezaji wa kwanza wa Chelsea kufanya hivyo tangu Ligi Kuu
ilipoanzishwa mwaka 1992.
Mlinzi huyo ambaye ameshatajwa kwenye kikosi bora
cha msimu cha Ligi Kuu (PFA Team of The Year) kwa mara ya nne, ‘amemtupia dongo’ (amemdhihaki) kocha wake wa zamani, Rafa
Benitez.
Benitez ambaye hakufikisha hata msimu pale Stamford
Bridge, alidai mlinzi huyo hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki.
Mafanikio haya binafsi ya Terry yanamuunganisha moja
kwa moja na Gary Pallister kama mchezaji ambaye si kipa kutokosa sekunde wakati
timu yake ikishinda taji la Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment