Straika wa Azam FC, John Bocco, amerejea rasmi juzi Jumatano na kuanza kujifua kwa ajili ya mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Simba baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na nyama za paja.
Bocco ambaye pia ni straika wa Taifa Stars alikuwa nje takriban wiki mbili ambapo alikosa michezo dhidi ya Stand United, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar na hii ni kutokana na maumivu ya nyama za paja.
Azam inatarajiwa kuvaana na Simba siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, huku wakiwa na pointi 45 na wapinzani wao wakiwa na alama 41.
Daktari wa Azam FC, Juma Mbaruku amesema kuwa kikosi hicho kinaendelea kupata matumaini baada ya nyota wake takriban watatu kuwa fiti wakiwemo Kipre Tchetche na Erasto Nyoni.
0 comments:
Post a Comment