Thursday, May 21, 2015


MWENYEKITI wa kikosi cha maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu Stars, Luteni Kanali Mnyani amewapongeza vijana wake chini ya kocha Fred Felix Minziro kwa kupambana kijeshi na kufanikiwa kubaki ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
JKT Ruvu Stars walinusurika dakika za mwisho wakimaliza katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wakijikusanyia pointi 31.
Kanali Mnyani katika pongezi zake pia amewapa ‘tano’ mabingwa wapya, Young Africans na kuwatakia kila la kheri kuelekea mechi za ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
“Kweli nimewapongeza vijana kwa kuweza kubakia ligi kuu, kadhalika nimewapongeza TFF, nimewapongeza bodi ya ligi, nimewapongeza mabingwa wetu wapya Yanga na kuweza kuwatakia kila la kheri katika mechi za kimataifa zilizopo mbele yao”. Amesema Kanali Mnyani na kuongeza: Bado tunajipanga, hivi karibuni tumepokea ripoti ya kocha na benchi la ufundi kwa ujumla, kwahiyo tunajipanga vizuri na taarifa tumeipokea jana tu, mambo mengine tutawafahamisha, jua usajili upo kama ilivyo kwa timu nyingine”.
Kocha Minziro amekuwa akilalamikia kitendo cha wachezaji wengi muhimu kupelekwa kwenye kozi za kijeshi wakati wa maandalizi na kuathiri programu zake za mazoezi pamoja na mechi za ligi kuu, lakini Kanali Mnyani amesema hilo wataliondoa msimu ujao.

“Kutakuwa na mabadiliko kwenye hilo, unajua sisi kama wanajeshi mbali na kucheza mpira tuna majukumu mengine ya ulinzi wa taifa letu, kwa safari hii tutajipanga ili isiweze kutokea tena”. Amesema Kanali Mnyani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video