Arsenal wako mbioni kuinasa saini ya mshambuliaji hatari wa Porto Jackson Martinez.
Mshambuliaji huyo raia wa Kolombia amekuwa kivutio kikubwa kwa mshabiki wa miamba hiyo ya Ureno tangu alipojiunga nao mwaka 2012, akifunga magoli 67 katika michezo 88.
Lakini tetesi kutoka vyanzo vya habari nchini Uingereza vinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa sana Arsenal wakafungua pochi yao ili kuinasa saini ya mpachika mbao huyo.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu nchini humo dhidi ya Penafiel ambao Porto walishinda 2-0, mashabiki walionekana wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa‘Obrigado Jackson’ wakimaanisha asante Jackson, wakiamini kuwa ule ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho kwa klabu hiyo.
Vyanzo vya taarifa hii ni magazeti ya Mirror, Metro na Daily mail.
0 comments:
Post a Comment