Na George Mganga, Dar es salaam
Wakati mwingine tujaribu kuvuta hisia na kukumbuka miaka ya nyuma nchi yetu ilikuwaje katika tasnia ya soka.
Ni mbinu gani ambazo zilitumika na kuiwezesha nchi yetu kupata heshima katika soka letu hapa Tanzania kabla hata mzee Mwinyi hajatamka lile neno lake la Tanzania kuwa ni kichwa cha mwendawazimu.
Sera ya soka kukua nadhani ilichangiwa pia na mfumo wa kukomaza vijana mapema tokea mashuleni wakiwa elimu ya Msingi.
Serikali wakati huo inaandaa hadi mashindano ya michezo mashuleni ilikuwa ikisaidia sana kuboresha na kuandaa hazina nzuri ya miaka ijayo hapa kwetu.
Sijajua sera hiyo imepotelea wapi maana hadi sasa michezo haijatiliwa mikazo katika elimu za juu.
Tanzania na kauli ya kichwa cha Mwendawazimu haitopotea endapo mipango na mikakati ya soka la kisasa haitaanzishwa na hili linalalia katika mfumo zaidi.
Tutazidi kulaumu makocha tu siku zote wakati mwingine makosa yanakuwa katika mfumo ambao unatumika vibaya na matakwa kwa wachezaji.
Uwepo wa wachezaji kutojitambua pia hata ile hamasa na motisha wanayopata kutoka kwa mashabiki wenye uchungu hawaioni.
Najiuliza maswali mengi bila kupata majibu juu ya hawa wachezaji wetu Wa Timu ya Taifa ya Tanzania, je ni wabovu au wanafanya makusudi?
Nimejitahidi kufuatilia mechi zote Tatu walizocheza huko Afrika Kusini, kiukweli timu imecheza chini ya kiwango kwa zaidi ya asilimia 70, kitu ambacho hakikutegemewa hapo kabla.
Malalamiko mengi yamekuwa yakielekezwa kwa mkufunzi Wa timu hiyo Mart Nooij, wengi wakisema kwamba hana mbinu lakini pia ameacha baadhi ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho.
Je, ni kweli hizo ni sababu zilizochangia Stars kufungwa mechi zote Tatu?
Hivi kweli hata kupiga pasi pia tunahitaji mwalimu akuelekeze?
Hakuna hata mchezaji mmoja aliyepiga pasi zenye uhakika kwa asilimia ishirini, wengi wao walikuwa wakipoteza pasi ovyo.
Nakubali kabisa kwamba kocha pia ana mapungufu katika mbinu zake za ufundishaji, mfano; katika mechi ya juzi baada kuona tumefungwa mabao mawili alimtoa kiungo na kumuingiza beki, mabadiliko ambayo sikuona umuhimu wake.
Lakini pia wachezaji wamekuwa hawaonyeshi juhudi zozote wakiwa ndani ya uwanja kwani wamekuwa wakicheza kama wagonjwa wengi wamelegea sana hawana nguvu ya kutosha lakini pia wanaonekana hawajui wanachokitafuta uwanjani.
Kila Mtanzania inabidi ajiulize je, ni kweli wachezaji wetu wanacheza vibaya kutokana na mbinu za kocha kuwa mbovu au wanafanya nakusudi?
Uongozi nao ni moja ya sehemu ambayo kila siku inatuhumiwa kuwa na umuzi wa kuunda kikosi maana hilo nalo NI kosa kubwa.
Unapomuondolea Mwalimu jukumu la kuandaa kikosi na kumpa majukumu yote ayafanye akiwa na timu, ndiyo hapo sasa tutaona uwezo fasaha wa mlengwa ambaye ndiyo Kocha.
Ifikie wakati sasa mipango madhubuti itumike kuiandaa Taifa Stars, maboresho yaanzie chini na mikakati kabambe iwepo.
Timu iwe na wachezaji wenye vipaji na sio kuchukua majina tu ambayo yamekuwa kama mapambo tu katika timu na sio majina ambayo yatakuwa mazuri katika upambanaji.

Kwa maoni, ushauri,tumia namba hii
0688665508.
0 comments:
Post a Comment