Timu
ya mpira wa kikapu ya Cairo kutoka Misri, jana ilikuwa kivutio kwenye uwanja wa
ndani wa Taifa baada ya kuamua kufanya ibada uwanjani wakati wa mapumziko wa
mechi yao ya nusu fainali dhidi ya timu ya Dar City ikiwa ni michuano ya mpira
wa kikapu inayoshirikisha timu za majiji ya Afrika Mashariki na Kati.
Mchezo
huo ulioanza majira ya saa 9:00 alasiri ulifika hatua ya mapumziko (half time)
saa 10:00 jioni muda ambao hutumiwa na waumini wa dini ya Kiislam kwa ajili ya
kufanya ibada (alasiri). Baada mwamuzi wa mchezo kupuliza filimbi kuashiria
mapumziko, wachezaji wa timu ya Cairo walikusanyika pamoja na kufanya ibada
uwanjani.
Kitendo
cha wachezaji hao kufanya ibada uwanjani kilionekana kuvuta hisia za mashabiki
wengi wa mchezo wa kikapu waliojitokeza kushuhudia pambano hilo. Imekuwa kama
utaratibu wa wachezaji wa kiarabu kufanya ibada viwanjani, kwani mara kadhaa
wameshuhutidiwa baadhi ya wachezaji wa Kiarabu hasa wa soka kushangilia kwa
kusujudu pale wanapofunga magoli.
Timu
ya Cairo ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa kuichapa timu ya Dar City kwa jumla
ya vikapu 92 kwa 60 na kutinga hatua ya fainali ambapo watakutana na timu ya
Qardho kutoka Somalia. Cairo ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo,
wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa fainali na kulitetea
kombe lao kutokana na mwenendo wao mzuri kwenye michuano hiyo ya siku tano.
Leo
itapigwa fainali ya michuano hiyo kwa kuanza na mchezo wa mshindi wa tatu
utakaopigwa majira ya saa 6:00 mchana ambapo Dar City itakuwa ikikabiliana na
Dar Stars, saa 8:00 mchana itachezwa fainali ya wanawake ambapo Kampala City
itapambana na Nairobi City wakati fainali ya wanaume itazikutanisha Cairo dhidi
ya Qardho mchezo utakaopigwa saa 10:00 jioni.
0 comments:
Post a Comment