Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm atarejea nchini
Juni 6 tayari kuanza kazi.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro amesema
Pluijm raia wa Uholanzi, mara moja ataanza mazoezi na timu hiyo baada ya
kurejea.
“Kocha kama mnavyojua yuko mapumziko, baada ya kurejea
ataanza kazi moja kwa moja. Lengo ni kuanza maandalizi mapema kabisa,” alisema Muro alipoongea na Salehjembe.
“Kuna michuano ya Kagame, pia kuna michuano mingine ya
kimataifa pia ligi kuu, hivyo lazima tuanza maandalizi mapema.”
Yanga tayari imeanza kufanya usajili kwa ajili ya kuimarisha
kikosi chake ambacho pamoja na michuano ya Kagame, kitashiriki ligi ya Mabingwa
Afrika.
0 comments:
Post a Comment