Nguli wa Arsenal Thierry Henry, amesema kuwa maoni yake dhidi ya Mfaransa mwenzake Olivier yalitafsiriwa vibaya.
Henry, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi katika runinga ya Sky Sports, alizua hali ya sintofahamu miongoni mwa mashabiki mara baada ya kusema, Arsenal hawawezi kuchua ubingwa kwa kumtegemea Giroud pekee mbele, badala yake wanahitaji mshambuliaji wa kiwango cha juu zaidi.
Baada ya hali hiyo Henry sasa ameamua kuifafanua kauli hiyo na kusema kuwa, alimaanisha kwamba Giroud anahitaji usaidizi mbele.
"Alexis Sanchez amenifanya niamini kuwa anaweza kuipeleka Arsenal mbali zaidi," Henry aliiambia Sky Sports. "Lakini ninachoamiani ni kwamba anahitaji usaidizi. Naamini pia Olivier Giroud anahitaji usaidizi.
"Nimesema nilichosema kuhusu Giroud na watu wakatafsiri tofauti. Wakati tulipokuwa tukishinda mataji ilikuwa ni kwa sababu Nwankwo Kanu alifanya vizuri wakati nilipokuwa nikihitaji mapumziko.
"Dennis Bergkamp, Sylvain Wiltord walikuwa mara nyingine wanapiga hat-trick, japo hawakuwa wakifanya hivyo mara kwa mara.
"Nadhani Arsenal wanahitaji mshambuliaji mwingine - hivyo ndivyo nilivyosema siku ile- ila ambaye ana utofauti na Giroud."
Henry aliongeza kuwa: "Nadhani wanahitaji kuboresha kikosi chao kwa kuongeza wachezaji wengine.
"Wakati nilipoongea kuhusu kuongeza ukubwa wa kikosi kwa kuongeza golikipa na mlinzi wa kati kiungo mkabaji na mshambuliaji , sina maana ya kwamba waliopo waondoke ili waje wapya ila namaanisha kuongeza ushindani."
0 comments:
Post a Comment