Si tu Raheem Sterling ambaye atatoa mkono wa kwaheri kuelekea mechi za kufunga msimu hapo kesho, wachezaji na makocha wa vilabu mbalimbali watakuwa wakionekana kwa mara ya mwisho kabisa katika vilabu vyao.
Didier Drogba anataraji kutoa mkono wa kwahaeri kwa klabu ya Chelsea baada ya kurejea klabuni hapa katika dirisha la majira ya joto msimu uliopita. Ikumbukwe tu Drogba ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na misimu mizuri kabisa akiwa na klabu hiyo.
Makocha
John Carver (Newcastle United). Alikuwa ni kocha wa muda wa klabu hiyo baada ya kuondoka kwa Allan Pardew. Vipigo nane kati ya michezo 10 ambayo klabu hiyo imecheza chini yake ni ishara tosha kuwa kocha huyo hana nafasi tena.
Sam Allardyce (West Ham United) Naye atatoa mkono wa kwaheri klabuni hapo huku timu yake ikiangalia kocha wa kumrithi.
Dick Advocaat (Sunderland) Bado ana hatihati ya kubaki hapo.
Wachezaji.
Danny Ings (Burnley) amefunga magoli 10 msimu huu na anataraji kusaini katika klabu ya Liverpool bure kabisa.
Didier Drogba (Chelsea) Anataraji kutoa mkono wa kwaheri kwa klabu ya Chelsea baada ya kurejea klabuni hapa katika dirisha la majira ya joto msimu uliopita. Ikumbukwe tu Drogba ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na misimu mizuri kabisa akiwa na klabu hiyo.
James Milner (Manchester City) Naye ni kusuka au kunyoa klabuni hapo.
Steven Gerrard anahitimisha kipindi cha miaka 17 ambacho ameitumikia Liverpool na kwenda nchini Marekani kujiunga na LA Galaxy
Charlie Austin (QPR). Kama alivyo mwenzake Ings, naye anatarajia kutimka QPR. QPR watashudia pia Shaun Wright-Phillips, Rio Ferdinand, Joey Barton, Richard Dunne, Bobby Zamora, Karl Henry, Clint Hill na Alejandro Faurlin wakiondoka pia.
David de Gea (Man Utd). Huyu yuko mbioni kutimkia nchini Uhispania kujiunga na klabu ya Real Madrid.
Brad Friedel anataraji kuondoka Tottenham baada ya mchezo wa kesho, huyu atavunja rekodi ya kuwa moja ya wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 44
Hugo Lloris (Tottenham). Huyu anaweza kwenda Man United kurithi mikoba ya De Gea endapo atatimkia Real Madrid.
Mario Balotelli naye ana hati hati ya kuondoka klabuni Liverpool kutokana na kiwango duni alichokionesha katika msimu mzima tangu aliposajiliwa kutoka AC Milan.
Frank Lampard (Man City) huyu anatarajia kuondoka Man City kwenda kujiunga na klabu ya New York City.
Petr Cech (Chelsea). Hana raha katika klabu ya Chelsea, yuko mbioni kutimkia ama klabu ya Arsenal au Manchester United.
Kiungo wa Man City, Yaya Toure ana hati hati ya kutimkia kunako klabu ya Inter Milan kuungana na kocha wake wa zamani Roberto Mancini.
Radamel Falcao atarudi katika klabu yake ya Monaco baada ya kumaliza kipindi cha cha mkopo katika klabu ya Man United, ambapo hakuonyesha kiwango cha kuvutia mara baada ya kufunga mabao 4, huku akiwa amewagharimu Man United paundi milioni 24.
...Na mwisho ni Waamuzi.
Chris Foy anatarajiwa kustaafu baada ya kutumikia kipindi chake cha uamuzi kwa miaka 14 akiwa ligi kuu nchini Uingereza pamoja na michuano mbalimbali ya Ulaya.
0 comments:
Post a Comment