STORI imeibuka kuwa Ilkay Gundogan jumatatu iliyopita alikuwa Barcelona akifanya ziara ya siri, kwa mujibu kwa gazeti la Bild.
Kiungo huyo alidhani atatumia faida ya FC Barca kutokuwepo mjini Barcelona kwa siku mbili zilizopita, hivyo asingeweza kunaswa na rada na kuwavutia watu wengi.
Gazeti la Bild halina uhakika kwa asilimi 100 kuwa alienda Barcelona kwa ajili ya matibabu kama ilivyodaiwa, lakini halikubali kuwa alikuwa pale kama mtalii na wanaamini mazungumzo baina ya Barcelona na mchezaji yamefanyika.
Karibia mwezi mmoja uliopita ripoti ziliibuka Ujerumani kwamba Gundogan amesaini Manchester United, lakini baadaye vyombo vya habari vya Ujerumani vikakanusha.
Kiukweli, United wanamuwinda nyota huyo, lakini Barcelona wana nafasi kubwa ya kuinasa saini yake.
Barcelona hawana uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote majira ya kiangazi mwaka huu kutokana na kufungiwa usajili na hii inamaanisha Gundogan atasubiri mpaka dirisha dogo la januari 2016.
0 comments:
Post a Comment