Friday, May 22, 2015

Olivier Giroud amejibu mapigo kwa  Thierry Henry kusema kuwa Henry alijihitajika kusema chenye utata ili kujizidishia umaarufu na kusisitiza yeye kama mchambuzi aliongea kitu chenye kukera.
Henry alitoa kauli kali lakini yenye ukweli juu ya Giroud kuwa mchezaji huyo ambaye pia ni raia wa Ufaransa kamwe hawezi kuipa Arsenal ubingwa wa EPL baada ya mechi kati ya Arsenal na Chelsea ambapo timu hizo zilitoka suluhu.
"Nadhani Giroud anafanya vizuri lakini je unaweza kuchukua ubingwa kwa kumtegemea yeye? Sidhani kama inawezekana,” Henry aliiambia Sky Sports.
“Nilimsikia akisema vitu vingi sana vya kuudhi. Lile lilikuwa ni bomu na lililenga moja kwa moja kwangu,” Giroud aliiambiaL’Equipe.
“Nilishangaa kumsikia akiiacha timu na kunitupia mzigo mimi. Nasema timu kwa sababu sikuwa peke yangu uwanjani, ila ilikuwa ni timu nzima. Hayuko sahihi hata kidogo.
“Sikufurahishwa na alichokisema. Kusikia hivyo kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Ufaransa na Arsenal, ni aibu kubwa, ilikuwa ni rahisi kwake kusema hivyo baada ya mchezo dhidi ya Chelsea.
“Tulikuwa tunafanya vizuri tu, tulicheza michezo kumi bila ya kupoteza, takwimu zangu zilikuwa nzuri. Inaniuma sana kushushwa thamani yangu.”
Giroud aliongeza kuwa, "labda Henry alihitaji kuona nikifikisha magoli 50 huku nikiwa nimecheza michezo michache zaidi yake.”
Giroud hajafunga tangu alipofunga katika mchezo dhidi ya Liverpool mwezi Aprili, ambapo Arsena walishinda kwaa magoli 4-1.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video