Sunday, May 17, 2015

GAZETI la leo jumapili la The Star limekuja na stori kwamba hatima ya Golikipa David De Gea kubaki Manchester United au kwenda Real Madrid itaamuriwa na familia yake.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la udaku, De Gea atafanya maamuzi yake wakati wa likizo baada ya kuitisha kikao cha familia yake mjini Madrid na inaelezwa kuwa kipa huyo anaheshimu mno mawazo ya familia katika maamuzi yake.
"Golikipa wa Manchester United bado hajafikia maamuzi ya kusaini mkataba wa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki Old Trafford au kujiunga na Real Madrid.
De Gea, 24, ana familia yake Hispania ambayo anaheshimu sana mawazo yake na ataomba maoni yao kabla ya kufikia maamuzi.
Mkutano huo unatarajia kufanyika baada ya ligi kuu England kuisha na utamuhusisha mpenzi wake anayeishi Madrid, Edurne Garcia.
Hata hivyo, gazeti la  Marca lilichapisha stori mwishoni mwa wiki iliyopita likidai De Gea tayari ameshamalizana na Real Madrid.
Kichwa kikubwa kiliandikwa ‘Trato Hecho’  katika ukurasa wa mbele pamoja na picha ya kipa wa Manchester United, David De Gea  kikimaanisha – ‘Done Deal’, yaani dili likemakilika.
Ngoja tubiri mwisho wa siku itakuwaje...........
Screen Shot 2015-05-17 at 9.21.16 AM

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video