WAZIRI Mkuu Mstaafu aliyejiuzulu
na Mbunge wa sasa wa jimbo la Monduli, Arusha, Edward Ngoyai Lowassa amesema
atahakikisha Tanzania inaondokana na msemo wa kuitwa ‘kichwa cha mwendawazimu”.
Lowassa ametamka
maneno haya wakati akihutubia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini
Arusha, akitangaza rasmi nia ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Lowassa ‘Mzee wa Maamuzi Magumu’ amese iwapo
atapitishwa kugombea kitu cha urais na kushinda basi atahakikisha anapambana na
udhaifu wa Tanzania katika michezo mbalimbali hadi kufikia kuitwa kichwa cha cha
Mwendawazimu.
"Kama nitapata nafasi,
basi nitahakikisha Tanzania inaondokana na kuitwa kichwa cha
Mwendawazimu," Amesema Lowassa na
kuongeza: "Tanzania tumekuwa hatufanyi vizuri katika michezo mbalimbali
ikiwemo riadha na michezo mingine."
Lowassa ni kati ya wanachama
wa CCM wanaowania nafasi hiyo ya urais kupitia CCM, wengine wanaotajwa ni
Benard Membe, Stephen Wasira, Mwigulu Nchemba na wengineo.
0 comments:
Post a Comment