John Terry akibeba kombe la ligi kuu England ambalo wametunukiwa leo Stamford Bridge wakimaliza msimu wa 2014/2015 kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Sunderland.
Chelsea ndio mabingwa wapya wa England na walitwaa ndoo hiyo mapema mwezi huu.
Loic Remy leo amefunga magoli mawili na moja limefungwa kwa mkwaju wa penalti na Diego Costa, wakati Steven Fletcher ameifungia Sunderland goli la kufutia machozi.

Raha za ubingwa hizo, pati limeanzia hapa...

Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba amepata heshima kubwa kutoka kwa wachezaji wenzake na mchezo wa leo ni wa mwisho kwake

Drogba akiwaongoza wenzake kushangilia ubingwa wa England

Hatimaye wachezaji wa Chelsea wamepata nafasi ya kushangilia na kombe



Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akiwaonesha ishara mashabiki wa Chelsea wakati wanajiandaa kubeba kombe
0 comments:
Post a Comment