Siku chache baada ya kusaini kuichezea Yanga, kiungo
mshambuliaji, Deus Kaseke, ametamka kuwa anaitumia timu hiyo kama njia kwake ya
kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya kwa kuwa Yanga itashiriki michuano ya
kimataifa.
Kaseke amesaini Yanga kwa mkataba huo wa miaka miwili kwa
dau la shilingi milioni 35 licha ya kuwindwa na Simba pia, amedai kuwa ndoto
zake zilikuwa ni kuichezea moja ya klabu kubwa nchini ili aonekane na apate
soko la kucheza nje ya nchi.
“Ilikuwa ni ngumu kwenda kusaini kuichezea Simba kwa ajili
ya msimu ujao na sijutii maamuzi niliyoyachukua ya kusaini Yanga kutokana na
malengo yangu niliyojiwekea katika soka.
“Ndoto zangu ilikuwa kuichezea timu itakayoshiriki michuano
ya kimataifa, hivyo ninaamini uwepo wangu Yanga utafungua milango kwangu
kuonekana kimataifa,” alisema Kaseke.
Yanga itashiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
kwa kuwa imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakati Simba ilishika nafasi ya tatu,
haitashiriki kimataifa katika michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka
Afrika (Caf) ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo.
0 comments:
Post a Comment