Didier Drogba akishangilia goli lake dhidi Leicester na sasa Chelsea wamekaribia kabisa kutwaa ubingwa
Chelsea na bodi ya ligi kuu England wamechukizwa na kitendo cha BBC kuonesha kombe la ligi kuu lililowekwa katikati ya duara la kati la uwanjani wa Stamford Bridge jumanne ya wiki hii.
Hii imetokana na Cheslea kutoamini wameshachukua ubingwa mpaka washinde mechi zijazo na Jose Mourinho amewaonya wachezaji wake na mashabiki akisema wanatakiwa kushinda kwanza dhidi ya Crystal Palace jumapili ya wiki hii kabla ya kushangilia ubingwa.
Watu 20 walishuhudia ziara iliyofanyika uwanja wa Chelsea na kuliona kombe kwenye uwanjani ingawa walinzi wa uwanja walijitahidi kulifunika lisionekane na kupigwa picha.
Jose Mourinho amewaonya wachezaji na mashabiki kujikita katika mechi dhidi ya Crystal Palace kabla ya kushangilia ubingwa
Bodi ya ligi kuu ilikubali ombi la BBC kurekodi video ya kombe Stamford Bridge kuwasaidia kufanya maandalizi ya mapema kabla ya Chelsea kucheza mechi mbili zijazo wiki hii.
Lakini imefahamika kuwa kombe hilo kubwa halikuonekana na watu wengi ambao wangeamini tayari Chelsea wamekuwa mabingwa.
Msemaji wa BB amesem: "Tulikuwa tunarekodi video kwa ajili ya kutumika siku ya kuwakabidhi kombe Chelsea, tulifanya kila juhudi kulifanya kombe lisionekane, lakini kwa bahati mbaya lilionekana kwa mbali wakati wa ziara ya uwanjani"
0 comments:
Post a Comment