Cheka (kulia) akidundana na Mthailand
Toka mwanzo wa pambano hilo tayari dalili zilionekana Cheka angeshinda kutokana na kummudu vyema mpinzani wake kwa kumsukumia makonde mazito mfululizo hali iliyomfanya Singwancha kuchoka mapema na kumwacha Cheka afanye anavyotaka kwa kumpiga kama begi la mazoezi.
Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza kwa Cheka toka abadilishiwe adhabu ya kifungo kutoka cha ndani (gerezani) mpaka kifungo cha nje. Ilipofika raundi ya nane, Singwancha alishindwa kuendelea na pambano baada ya kupigwa vilivyo na kuamua kukubali kushindwa hivyo mwamuzi wa mchezo huo Anthon Ruta kulivunja bambano hilo na ushindi ukaenda kwa Cheka.
Baada
ya pambano kumalizika Cheka alisema kuwa, amepigana pambano hilo bila kujua
kama atapata pesa yake au la, lakini aliamua kupanda ulingoni kwa ajili ya
kuwaridhisha mashabiki wake walijitokeza kwenye pambano hilo tofauti na
angeamua kugomea.
“Namshukuru
mwenyezi Mungu nimeweza kufanya vizuri kwenye pambano langu, lakini nawashukuru
pia mashabiki wangu na waandishi wa habari, mnajitahidi sana kututangaza”,
alisema Cheka.
“Pambano
hili nimepigana kwangu mimi halina hata pesa lakini nimepigana kwa ajili ya
mashabiki wangu ili waweze kuona ni kwa jinsi gani nipo fiti, salama na nauwezo
wa kufanya vizuri kama watapatikana ‘masponsor’ wengine wakubwa. Angalia
promoter Kaiki Siraji amejitahidi lakini hela ya kunilipa sasahivi hana”, Cheka
alifafanua.
“Ningeweza
kukataa kucheza lakini ningewapoteza mashabiki wangu, na mimi nawapenda
mashabiki wangu. Kwa uwezo wangu na kwa juhudi zangu binafsi niliweka kambi
mimi na kocha wangu kwa gharama zangu mimi mwenyewe lakini nikaja kusaidiwa kwa
siku tatu ambazo nimekuwepo hapa Dar es Salaam”, aliongeza Cheka.
“Mapromota
wanategemea pesa ya viiingilio vya mlangoni ili waweze kutulipa, sasa mimi
nadai shilingi milioni nne, sasa hapa kunakupewa milioni nne kweli. Maana hata
milioni mbili haipatikani, sasa kwangu mimi iko hivi itakuwaje kwa hawa
mabondia wadogo wanaopigana kwenye mapambano ya utangulizi?”,Cheka alihoji.
Kwa
upande wake Singwancha, amekubali kushindwa pambano lakini akasema kushindwa
kwake kunatokana na kupata majeraha kwenye mkono wake wa kulia wakati akiwa
mazoezini na kusababisha kutumia mkono wa kushoto pekee.
“Nimekubali
kupoteza mchezo dhidi ya Cheka lakini hii inatokana na kuumia mkono wangu wa
kulia na kunilazimu kutumia zaidi mkono wa kushoto kwa mambo yote, kujilinda na
kushambulia. Unapotumia mkono mmojazaidi, unapoteza balance hivyo unatoa mwanya
kwa mpinzani wako kufanya vile anavyotaka”, alisema Sengwancha.
0 comments:
Post a Comment