Tuesday, May 26, 2015

Chanongo mwenye jezi namba 8 kwenye bukuta yake

WINGA aliyekuwa anakipiga kwa mkopo Stand United akitokea Simba, Haruna Chanongo amesema majeruhi ndio sababu ya yeye kushindwa kwenda TP Mazembe ya DR Congo kufanya majaribo ya soka la kulipwa.
TP Mazembe wanayochezea Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu walimualika Chonongo kujaribu bahati yake ya soka la kimataifa.
Chonongo ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba, ameuambia mtandao huu kuwa mipango yake ilikuwa ni kuondoka mara tu baada ya ligi kuu kumalizika mei 9, lakini majeraha yamemurudisha nyuma.
"Mipango yangu ilikuwa nikimaliza ligi nienda kimataifa, lakini tofauti na nilivyofikiria, nikipata majeruhi na kushindwa kwenda nje kufanya majaribio na TP Mazembe". Amesema Chanongo.
Siku za karibuni iliripotiwa kwamba Chonongo amesajiliwa na Yanga, lakini meneja wake Jamal Kasongo akakanusha taarifa na kueleza kuwa wamewasiliana tu na Yanga.
Mtandao huu umemtafuta mchezaji mwenyewe (Chanongo) ambaye pia amekanusha kusajiliwa na Yanga.
"Taarifa za kumalizana na Yanga si za kweli, lakini wao waliongea na mwanasheria wangu (Jamal Kisongo) na mpaka sasa hivi sijasaini Yanga" Amefafanua Chonongo.
Kuhusu mustakabali wake wa msimu ujao, nyota huyo amesema: "Nikipata timu yoyote ya Tanzania nipo tayari kuichezea, kikubwa ni maelewano"

Chanongo aliumia Aprili 21 mwaka huu uwanja wa Taifa, Stand United ikichapwa 3-2 dhidi ya wenyeji Yanga na madhara yake akakosa mechi tatu dhidi ya Azam fc ambayo walifungwa 4-0, Coastal Union ambapo walifungwa tena 3-1 na Ruvu Shooting waliyoshinda 1-0 wakifanikiwa kubaki ligi kuu msimu ujao.
Lakini amesema kwasasa anaendelea vizuri na juma lijalo ataanza mazoezi madogo madogo.
"Namshukuru Mungu naendelea vizuri ingawa bado sijaanza mazoezi madogo madogo, natarajia kuanza jumatatu au jumanne ijayo". Amesema Chanongo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video