Arsenal wamefungua milango ya majadiliano juu ya kumnyakua mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech kwa ada ya paundi milioni 10.
Paris Saint-Germain pia wanaonekana kuwa na nia ya kupata saini ya mlinda mlongo huyo mkongwe na mwenye mafanikio klabuni hapo.
Lakini Arsenal wanaonekana kuwa na nafasi kubwa sana kutokana na ukweli kuwa Mlinda mlango huyo hataki kuisumbua familia yake kwa kuhamia mahali pengine isipokuwa kubaki katika jiji la London.
Mourinho kwa upande wake amesema asingependa kuona Cech anajiunga na Arsenal lakini maamuzi ya mwisho yapo kwa mlinda huyo mwenyewe.
Wakala wa Cech Viktor Kolar amesema: ‘Arsenal, Manchester United au PSG ni miongoni mwa timu zinazopigana vikumbo kuwania saini ya Cech huku akiongeza kuwa, Cech mwenyewe anaamini kuwa maamuzi ya mwisho yapo kwa Roman Abromovich na si kocha wa klabu yake Jose Mourinho.
0 comments:
Post a Comment