Kipigo cha magoli 6-1 walichokipata Liverpool kutoka kwa Stoke City kimeamsha hasira kubwa wapenzi, wachezaji wa zamani pamoja na mashabiki wa klabu hiyo.
Kipigo hicho kimeweka mashaka kibarua cha Brendan Rodgers huku kukiwa na tetesi kuwa anaweza kutimuliwa klabuni hapo na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp.
Katika ukurasa wake wa twitter beki wa Zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa kituo cha rininga cha Sky Sports Jamie Carragher aliandika hivi:
"Embarrassing day for all connected with LFC 6-1 is not acceptable."
Akimaanisha;Ni aibu ya siku kwa wote wanaohusika na Liverpool, magoli 6-1, haikubaliki hii.
"Sikuona chochote zaidi ya mwanangu kutoka uwanjani katika nusu ya kwanza ya mchezo, ni mbaya sana hii!!"
Naye Brendan Rodgers baada ya mchezo alisema hivi;
"Mashabiki wahahitaji kuombwa radhi kwa hili. Tumefungwa kirahisi mno. Tunatakiwa kuwa bora zaidi yao."
"Mashabiki watakuwa na hasira sana na wana haki ya kuwa hivyo.
"Mimi kama kocha nitawajibika kwa hili. Kuna kazi kubwa sana ya kufanya. Tumemaliza nafasi ya sita na ndipo tunastahili kuwepo.
"Kama wamiliki watataka niondoke, basi naondoka. Ni rahisi tu kama hivyo. Lakini nadhani bado nina mengi ya kufanya hapa."
0 comments:
Post a Comment