Nadir Haroub (kushoto)
KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amemuondoa kikosini nahodha wake Nadir Haroub 'Cannavaro' baada ya kubaini kuwa bado hayuko fiti kucheza mechi hiyo.
Kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema 'bosi' wake amemuanzisha kipa Deogratius Munish golini, Juma Abdul ameanza kulia, Oscar Joshua kushoto, walinzi wa kati watacheza Mbuyu Twite na Kelvin Yondani na mbele yao watacheza Juma Said Makapu. Hiyo ndiyo safu ya ulinzi baada ya Cannavaro kutolewa kikosini.
Salum Telela ataichezesha timu, wakati Amissi Tambwe, Simon Msuva , Kpah Sherman na Mrisho Ngassa wataanza safu ya ushambuliaji.
"Yanga ina wachezaji wengi, tumeweza kumuondoa Cannavaro, hapa kuna baridi sana, kumchezesha inaweza kumuongezea maumivu, kama ataumia maana yake tutafanya mabadiliko ya lazima. Bora akae nje tu, Mbuyu (Twite) na Yondani (Kelvin) tumewapa majukumu katikati, mbele yao atacheza Makapu (Juma Said) ni wachezaji wazuri". Amesema Mkwasa.
0 comments:
Post a Comment