Friday, May 1, 2015


Cannavaro (kushoto) ndiye alifunga goli kwa penalti katika sare ya 1-1 na Etoile du Sahel
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kukosa mechi tatu za ligi kuu Tanzana bara kesho anatarajia kuongoza ngome ya ulinzi dhidi ya Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Cannavaro alipata majereha katika mechi ya awali ambayo Yanga na Etoile du Sahel zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa, Dar es salaam aprili 18 mwaka huu.
Mlinzi huyo wa timu ya taifa ya Zanzibar na Taifa Stars aliikosa mechi dhidi ya Stand United ambayo Yanga walishinda 3-2,  akaikosa mechi ya Ruvu Shooting ambayo Yanga walishinda 5-0 akaikosa mechi iliyopita dhidi ya Polisi Morogoro ambayo Yanga walitangaza ubingwa kwa kushinda 4-1.
Cannavaro ambaya atasaidiana na Kelvin Yondan kesho amewaomba Watanzania wote kuwaombea Yanga dua njema ili waweze kuwatoa Etoile.
“Kwanza tunashukuru Mungu tumefika salama, la pili tuna mechi ngumu kesho, lakini sisi tumejiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho. Tunawaomba Watanzania wote watuombee dua japokuwa wao hawapo katika mji wa Tunisia, lakini dua zao zinaweza kutusaidia”. Amesema Cannavaro akiwa nchini Tunisia.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video