Timu
ya Cairo kutoka Misri imefanikiwa kutetea taji lake la ubingwa wa mpira wa
kikapu wa michuano ya majiji ya Afika Mashariki na Kati (East & Central
Africa Inter-Cities Championship) baada ya kuifunga timu ya Qardho ya Somalia
kwenye mchezo wa fainali uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Mchezo
huo ulioshuhudiwa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiongozwa na Balozi wa
Misri nchini Tanzania pamoja na mama wa nyota wa mchezo huo Hasheem Thabiti.
Pambano hilo lilikuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote mbili kuonesha
viwango vya juu hali iliyoufanya mchezo huo kuwa mkali na wakuvutia zaidi.
Cairo
ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuifunga timu ya Qardho kwa jumla ya vikapu
79 kwa 59 na kutetea taji hilo ambalo walilitwaa pia mwaka uliopita. Mechi hiyo
ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa kikapu kutokana
na timu hizo kutoa vipigo vikali kwa timu za Tanzania hivyo ilikuwa ikisubiriwa
kuona nani ataibuka mbabe na kutwaa ubingwa huo kati ya timu hizo mbili.
Kwa
upande wa wanawake, timu ya Nairobi City imenyakua ubingwa baada ya kuilaza
timu ya Kampala City wakati timu za Tanzania zimeendelea kuwa wasindikizaji
kwenye michuano hiyo mikubwa ya kikapu kwa ngazi ya majiji ya Afrika Mashariki
na Kati.
Mashindano
hayo yaliyoshirikisha jumla ya timu10 kutoka kutoka nchi za Afrika Mashariki na
Kati. Nchi hizo zilikuwa ni pamoja na Tanzania ambao walikuwa wenyeji, Kenya,
Uganda, Somalia pamoja na Misri yalianza Mei 27 na leo Mei 31 ndio ilikuwa siku
ya kufunga pazia la michuano hiyo ambapo inatarajiwa kufanyika mwaka ujao kwa
mara nyingine.
0 comments:
Post a Comment