Friday, May 22, 2015

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Liverpool, Rafael Benitez ameonyesha kufurahishwa na tetesi zinazoendela katika vyombo vya habari baada ya jina lake kuhusishwa na mchakato wa kuirithi nafasi ya Carlo Ancelotti huko Stantiago Bernabeu.
Benitez ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha SS Napoli, amesema amefarijika kusikia habari hizo kupitia vyombo vya habari, japo maamuzi ya mwisho yatatolewa na viongozi wa klabu hiyo ambayo imetoka kapa msimu huu, baada ya kushindwa kutwaa taji la michuano yoyote.
Hata hivyo wakala wa Rafael Benitez, ameungana na mteja wake katika suala hilo lakini akaonyesha kuwa na shaka na taarifa za vyombo vya habari kwa kusisitiza subra zaidi, kufuatia uongozi wa klabu ya Real Madrid kutotoa kauli ya jambo hilo mpaka sasa.
Manuel Garcia Quilon, wakala wa meneja huyo mwenye umri wa miaka 55 ameendelea kubainisha kwamba Benitez ni meneja ambaye anakidhi vigezo vinavyostahili kuiongoza klabu kama ya Real Madrid hivyo hana shaka na jambo hilo, endapo tetesi hizo zitakuwa za kweli.
Carlo Ancelotti amekuwa akitajwa kama muhanga wa matokeo mabovu huko Estadio Stantiago Bernabeu, siku chache baada ya kikosi cha The Meringues kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kufungwa jumla ya mabao matatu kwa mawili dhidi ya Juventus.
Lakini meneja huyo kutoka nchini Italia, amekuwa akihusishwa na mipango ya kuwa na uhakika wa kupata ajira, endapo ataamuriwa kuondoka mjini Madrid huku klabu za Man City pamoja na AC Milan zikitajwa kuwa mastari wa mbele katika mkakati huo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video