BASI la wachezaji wa timu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara, ambalo lilikuwa linatumika kusafirisha wachezaji kwenda sehemu mbalimbali kucheza mechi za ligi kuu soka Tanzania limewekwa bondi baada ya kushindwa kulipa gharama ya Hoteli waliyokuwa wanalala wachezaji hao kwa muda wa miezi miwili.
Ndanda 'Mtwara Kuchele' wanadaiwa jumla ya milioni kumi na mbili (12) ambayo wamepunguza hadi kufikia milioni saba, laki moja na sitini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mtwara, (MTWARAREFA), Mwenyekiti wa chama hicho, Athumani Kambi, amesema basi hilo limezuiliwa kutolewa kwenye Hoteli ya Peninsula kutokana na kushindwa kulipa deni hilo kwa wakati.
Hata hivyo Kambi amesema kwa sasa ameamua kuachia ngazi ya Ukurugenzi aliyokuwa nayo kwenye timu hiyo ya Ndanda FC kwasababu ya kutingwa na majukumu mengine ya kikazi.
Kwa upande wake Afisa habari wa timu ya Ndanda Fc, Idrisa Bandali amesema kitendo cha Kuachia ngazi kwa Kambi aliyekuwa Mkurugenzi wa timu hiyo kimemshitua sana kwani alikuwa anaisaidia timu zaidi.
0 comments:
Post a Comment