Thursday, May 21, 2015


Katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii jana baada ya Taifa Stars kung'olewa Cosafa kwa kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya Madascar, nilisoma maoni mengi mno na waliowengi wanamshambulia kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Mart Nooij hususani katika uteuzi wa kikosi cha hovyo.
Lakini mwisho wa reli, mdau mmoja kwenye kundi moja la michezo la Facebook ambaye amekerwa na matokeo ya Stars,  amemuandikia barua ya wazi, Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Alhaj Ally Hassan Mwinyi.
Jisomee barua hiyo, nimeichukua kama ilivyo:
...............................................
AWALI YA YOTE KWANZA KABISA NAPENDA KUKUPA HESHIMA YAKO MZEE WANGU , RAIS WANGU MSTAAFU ALHAJ ALLY HASAN MWINYI, SHIKAMOO MZEE.


NIA NA DHUMUNI LA BARUA HII NI KUKUTAKA WEWE UKIWA KAMA MZEE WETU KUTENGUA KAULI YAKO ILEEE ULIYOSEMA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.

KUMBUKA MZEE WANGU MANENO YA MTU MZIMA YAKITOKA HUWA HAYARUDI MATUPU .
VIJANA WAKO TUNATAABIKA NA KAULI YAKO KWA MAANA MPAKA LEO INATUTAFUNA.

ALHAJI MWINYI TUNAKUOMBA KWA MOYO MKUNJUFU TENGUA KAULI YAKO YA KUWA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU ILI KULINUSURU TAIFA KATIKA MASWALA YA MICHEZO HUSUSANI MPIRA WA MIGUU.

MZEE WETU HIVI SASA TUPO KATIKA HALI MBAYA KULIKO VILE KABLA HUJATOA KAULI YAKO KWA MAANA HAPO MWANZO TULIKUWA TUNAJIKONGOJA YANI UAFADHALI ULIKUWEPO.

ZAMANI TIMU ILIKUWA HAINA MAANDALIZI MAZURI KAMBI ILIKUWA INAWEKWA JESHI LA WOKOVU , WACHEZAJI WANAENDA MAZOEZINI NA DALADALA HUKU POSHO KUKIWA HAKUNA ILA WALIPIGANA NA KUILETEA NCHI HESHIMA.

MUHESHIMIWA TANGU UTOE KAULI YAKO ILE TAIFA STARS IMEKUWA KWELI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.

HAKUNA WA KUINUSURU TAIFA STARS ZAIDI YAKO WEWE
MUHESHIMIWA ALHAJ ALLY HASANI MWINYI.

ONA MUHESHIMIWA LEO HII TUNAFUNGWA NA NCHI AMBAYO
MFALME WAKE HANA ANACHOWAZA ZAIDI YA KUOA VIGORI KILA MSIMU UFIKAPO.

MUHESHIMIWA TUNAKUOMBA TENA NA TENA YANI TUPO CHINI YA MIGUU YAKO TENGUA KAULI YAKO ILI KUINUSURU STARS YETU.
SINA MENGI ZAIDI MZEE WANGU ILA NATUMAI UJUMBE WANGU
UTAKUFIKIA NA UTAUFANYIA KAZI.
WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA.
*****    wako mimi   ******

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video