Jose Mourinho
amesisitiza kuwa Barcelona na Real Madrid zingekutana na kibarua kigumu
kushinda kombe la ligi kuu England.
Soka la
Hispania halimridhishi Mourinho akidai halina ushindani licha ya yeye kushinda kombe la La Liga kwa rekodi ya pointi
mia moja na magoli 121 mwaka 2012 akiwa kocha wa Real Madrid.
Chelsea wametawazwa
mabingwa wa ligi kuu zikisalia mechi
tatu, lakini Mourinho anadai wamefikia mafanikio kwa kutoa jasho kwasababu
England hakuna vitu rahisi kama La Liga.
Mourinho
amesisitiza kuwa alipokuwa Hispania hakuwa na furaha kwasababu alitwaa ubingwa
kwa rekodi ya pointi na magoli mengi, lakini alicheza mechi nne au tatu kwa
msimu mzima. Pia alipoteza ubingwa kwa pointi 92 huku akicheza tena mechi nne
au tano kwa msimu mzima.
0 comments:
Post a Comment