Messi akishangilia goli la ubingwa
LIONEL Messi amewapa Barcelona ubingwa wa La Liga msimu wa 2014/2015 baada ya kuifungia bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicent Calderon.
Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65' akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja.
Real Madrid wameshinda magoli 4-1 dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 katika mechi 37 walizocheza.
Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona .
Inawezekana msimu ukawa mkubwa kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu, La Liga na watacheza fainali mbili, ligi ya mabingwa ulaya na kombe la mfalme 'Copa del Rey'.
Licha ya kuugulia maumivu ya kutolewa nusu fainali ya Uefa na Juvuntes katikati ya wiki hii na leo kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji hatari wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu peke yake 'hat-trick' katika ushindi wa Madrid.
Ronaldo amefunga magoli hayo katika dakika ya 59', 83' na 90'. Goli lingine limefungwa na Marcelo dakika ya 79' wakati goli la kufutia machozi kwa Espanyol limefungwa na Cristian Stuani dakika ya 73''.
MATOKEO YOTE YA LA LIGA USIKU HUU HAYA HAPA:
FT
0 comments:
Post a Comment