KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Liewig amesema yuko tayari
kurejea nchini na kuinoa Simba.
Liewig amesema anajisikia faraja kama
atapata nafasi hiyo ili atimize ndoto yake. Pia yuko tayari wakati wowote kwa
ajili yao.
“Wakati ule niliondoka nikiwa ndiyo nimeanza kufanya kile
nilichokuwa nimekitaka.
“Kikosi changu hakikuwa kimefanya kazi vizuri mwanzoni.
Baada ya kambi ya Oman kulikuwa na mabadiliko kadhaa. Nikaona ndiyo timu
inaanza kuonyesha njia, nikaondolewa.
“Nikipata nafasi hiyo kwa sasa nina imani nitafanya vitu
vizuri kwa kuwa Simba ina watu wengi wanajua mpira,” alisema Liewig.
Mfaransa huyo aliingoza Simba kwa nusu msimu, tena ikiwa na
kikosi chenye vijana wengi sana.
Simba iko katika harakati za kusaka kocha mpya baada ya
Goran Kopunovic “kuzingua” kwa kudai dau kubwa ambalo Simba wameona hawaliwezi.
0 comments:
Post a Comment