Jonas Gutierrez ameibwatukia klabu yake ya Newcastle baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Muargentina huyo hatapewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Ilithibitishwa rasmi katika tovuti ya klabu hiyo kuwa Gutierrez, pamoja na Ryan Taylor, hawatapewa mikataba mipya na hivyo kuondoka klabuni hapo pindi mikataba yao itakapomalizaika Juni 30.
Gutierrez alirudi kundini mara baada ya kupona maradhi yake ya kansa ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu na kufanikiwa kupigania nafasi ya timu yake kubaki katika ligi kuu kwa msimu ujao.
Winga wa Newcastle Jonas Gutierrez akisherehekea baada ya kuifungia timu yake goli la pili dhidi ya West Ham na kuafaikiwa kuibakisha klabu yake ligi kuu.
Gutierrez ameichezea Newcastle michezo 205 tangu alipowasili klabuni hapo mwaka 2008.
Gutierrez, akisherehekea ushindi na kocha wake John Carver, baada ya kurudi kutoka na kupona maradhi ya kansa yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu msimu huu.
Baada ya taarifa hizo za kuachwa na Newcastle kumfikia Gutirrez, aliandika hivi kwenye akaunti yake ya Twitter jana usiku:
'Two things I learn from my illness how you can support a player (newcastle fans) and how you leave a player alone (newcastle owner).
Akimaanisha kuwa:'Vitu viwili nimejifunza kutokana na maradhi yangu, cha kwanza ni namna gani ya kumsapoti mchezaji(hii ni kwa upande wa mashabiki wa Newcastle) na namna gani ya kumuacha mchezaji peke yake (hii ni kwa upande wa wamiliki wa Newcastle)'
0 comments:
Post a Comment