Monday, May 25, 2015


Kaseke akiongea na waandishi wa habari baada ya Yanga kumtambulishwa rasmi leo

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Dida, kipa chaguo la kwanza la Taifa Stars kwa sasa, amekuwa akiwania na Simba kwa muda mrefu.'

HUKU wakiwazidi kete wapinzani wao wa jadi Simba kwa kumwongeza mkataba wa miaka miwili kipa Deogratius Munishi 'Dida', Yanga wamemtambulisha rasmi mchezaji wao mpya Deus Kaseke aliyetua Jangwani mwishoni mwa wiki akitokea Mbeya City.

Dida, kipa namba moja wa Taifa Stars kwa sasa, alikuwa anawatoa udenda vigogo wa Simba ambao hivi karibuni walionyesha nia ya kumsajili, lakini sasa watalazimika kusuburi au kuvunja mkataba wake mpya na mabingwa hao mara 25 wa Tanzania Bara.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, amesema kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam leo mchana kuwa Kaseke, kiungo mshambuliaji aliyeng'ara katika kikosi cha City misimu miwili iliyopita, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani.

Muro amesema kusajiliwa kwa nyota huyo aliyekuwa anawaniwa kwa udi na uvumba na Simba, kumetokana na pendekezo la kocha mkuu Mdachi Hans van de Pluijm akiamini atasaidia kuziba moja ya namba zilizo wazi za winga wa kulia mshambuliaji wa kati na winga wa kushoto.

"Kocha (Pluijm) kabla ya kuondoka aliacha mapendekezo yake ya wachezaji gani anaowataka na sisi kama uongozi tumeutilia maanani na tumefanya kama tulivyoagizwa," amesema Muro.

"Mbali na Kaseke, klabu imesaini mikataba mipya na kipa Deogratius Muinish 'Dida', ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka miwili, Mbuyu Twite amesaini mwaka mmoja na Haruna Niyonzima amesaini mkataba mpya wa miaka miwili," ameeleza Muro huku akiongeza kuwa bado wapo kwenye mikakati ya kuendelea na usajili wa wachezaji wakali waliopendekezwa na kocha.

KASEKE AFUNGUKA
Baada ya kutambulishwa rasmi leo, Kaseke ameahidi kufanya mambo mazuri ndani ya Yanga kwa vile klabu hiyo ilikuwa katika ndoto zake.

"Naahidi kufanya makubwa katika timu yangu mpya kwani siku zote nilitamani kuonesha uwezo wangu katika michuano mikubwa", amesema Kaseke.

Amesema kuwa anatambua kuwa amesajiliwa na klabu hiyo ili kuziba nafasi ya winga hatari, Mrisho Ngassa, aliyetimkia klabu ya Free State inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Kaseke alikabidhiwa jezi namba nne (4) ambayo ilikuwa inavaliwa na beki wa kati, Rajab Zahir.

YANGA KAMBINI JUNI 8
Katika hatua nyingine, Hafidh Saleh, meneja wa timu ya Yanga, amesema kuwa kikosi chao kinatarajiwa kuanza mazoezi Juni 8 kwenye shule ya sekondari Loyola uliopo Mabibo jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa michuano ya Kombe la Kagame.
Yanga itashiriki michuano hiyo  mwaka huu ikiwa ni moja ya timu wenyeji wa michuano hiyo ambayo inafanyikia nchini. mwezi ujao.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video