Wakati
dunia ikijadili kama maamuzi ya Steven
Gerrard kwenda La Galaxy ya Marekani ni sahihi, baba mzazi wa Xavi Hernandez,
Joaquim Hernandez amesema mwanae ataondoka Barcelona kwenda kumalizia soka lake
katika klabu ya Al Sadd ya Quatar.
Xavi
ambaye amecheza Barcelona tangu akiwa mtoto kwa miaka ya karibuni hana namba ya
kudumu katika kikosi cha kwanza, lakini ni miongoni mwa mashujaa wa kikosi cha
Hispania waliotwaa ubingwa kombe la mataifa ya Ulaya na dunia.
Baba
mzazi wa Xaiv amesema tayari maamuzi yameshafikiwa na kilichobaki ni mwanae
kuaga, huku akifichua kuwa katika mkataba anaotarajia kusaini Al Sadd unamruhusu
kuwa kocha mchezaji.
Hata
hivyo taarifa za ndani kutoka Barcelona zinasema kiungo huyo mkongwe atafanya
mkutano wa kuaga na waandishi wa habari alhamisi ya juma hili.
Mkataba
wa Xavi na mabingwa hao wapya wa Hispania unamalizika mwakani, lakini ameamua
kuondoka zake baada ya msimu huu kumalizika.
0 comments:
Post a Comment