Thursday, May 21, 2015

AZAM FC wanasuasua kumtangaza rasmi Muingereza Stewart John Hall kuchua nafasi ya kocha aliyeachishwa kazi, Mcameroon, Joseph Marius Omog.
Stewart na Azam kimsingi wamemalizana, kilichobaki ni kutangazwa rasmi pamoja na wasaidizi wake ambao tayari wameshasaini mikataba mipya, George ‘Best’ Nsimbe (msaidizi namba moja) na Dennis Kitambi (msaidizi namba mbili).
Kinachochelewesha kutangazwa kwa Stewart ni kumsubiri amalizane na waajiri wake, Symbion Power ambapo anafanya kazi kama mkurugenzi wa kituo cha soka cha vijana kinachojengwa na kampuni hiyo  jijini Dar es salaam.
Stewart aliwaandikia Symbion barua ya kuomba kuacha kazi ‘Notice letter’ ya siku 30 na akimalizana nao ataanza kazi rasmi Azam fc juni 15 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Azam fc, Nassor Idrissa ‘Father’ amesema siku si nyingi watamtangaza kocha mpya ambaye hajataka kumtaja, lakini hakuna shaka yoyote ni Stewart kwa asilimia 100.
“Suala la kocha litamalizika baada ya siku mbili zijazo, tunataka kutangaza kitu kilichokamilika, kutangaza kuwa tumeingia kandarasi na kocha fulani nafikiri ni siku mbili, tatu tu zijazo”. Amesema ‘Father’ na kusisitiza: “Suala la mchezaji au kocha sio la kificho, lakini kama unavyojua masuala yao ni ya kimkataba na sheria, sisi kama klabu hatuwezi kupaza sauti zetu moja kwa moja wakati mambo ya kimkataba hayajakaa sawa, muda mchache ujao tutaweka kila kitu  hadharani”

“Walimu ambao tumekaa nao kwenye meza ni pamoja na mwalimu Stewart Hall, tutawatangazia kama ni yeye anachukua nafasi au mwingine”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video