Radio Praha ya jamhuri ya Czech imeripoti kuwa Arsenal wanakaribia kumsajili kipa mkongwe wa Chelsea, Petr Cech.
Baada ya Thibault Courtois kuwasili darajani majira ya kiangazi mwaka jana, Cech kwa karibu msimu mzima amekaa benchi akicheza mechi za makombe ya nyumbani tu na mechi chache za ligi kuu England zisizokuwa muhimu.
Ni anguko la ghafla kwa kipa huyo wa Jamhuri ya Czech ambaye alikuwa mlinda mlango namba moja Chelsea asiyeguswa kwa muongo mmoja na akishinda kila kombe.
Kufuatia kuona hali ya mambo msimu huu na kupima upepo, Cech ameamua kuondoka zake akitafuta timu nyingine atakayokuwa kipa namba moja na amekuwa akihusishwa kujiungana wapinzani wa London wa Chelsea, Arsenal kwa dau la paundi milioni 10.
Hata hivyo,Jose Mourinho anapingana na dili hilo akidai huko ni kuwaongezea nguvu wapinzani wake wa moja kwa moja, lakini Cech na wakala wake ndio wanaweza kuwa na neno la mwisho juu ya suala hilo.
0 comments:
Post a Comment