Saturday, May 2, 2015

KOCHA wa Real Madrid Carlo Ancelotti ametanabaisha kuwa ana matumani makubwa ya kuwa na Gareth Bale katika mchezo leo dhidi ya Sevilla, Bale alikuwa nje akiuguza jeraha la kweye nyama za mguu lililokuwa likimsumbua kwa takribani wiki tatu.
Hata hivyo Ancellotti ameshindwa kuthibitisha kati ya Bale na Karim Benzema ambaye naye alikuwa nje akiuguza jeraha la goti kuwa nani ataanza katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Ramon Sanchez Pizjuan.
"Nadhani Bale yuko vizuri kwa sasa," alisema. "Nina machaguo mengi sana tu katika eneo la kiungo, nadhani nitafanya maamuzi wakati wa kupanga kikosi.
"Bale na Benzema wako timamu kabisa? hatuwezi kuwalazimisha kucheza. Huu sio mchezo wa mwisho katika ligi msimu huu.
"Kama mchezaji yuko vizuri basi atacheza. kweli hawawezi kucheza dakika zote 90 lakini wapo fiti.
"Lakini hata hivyo hatuko tayari kuwalazimisha kucheza, tunajali afya zao, " alimaliza Ancellotti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video