Saturday, May 23, 2015

Kocha wa Juventus  Massimiliano Allegri amesema kuwa, atahakikisha anaiharibu siku ya kiungo mahiri wa Barcelona Xavi Hernandez, pale timu yake itakapokutana na Barca katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa Ulaya utakaopigwa Juni 6, ambapo huo ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho kabla ya kutimkia  Al Sadd ya Qatar.
"Utakuwa ni mchezo wa mwisho kwa Xavi,mchezaji wa aina yake ambaye amewahi kutokea Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, lakini tunatumaini kuwa tutamuharibia sherehe yake," Allegri aliwaambia waandishi.
"Najua kuwa Barca wana wachezaji hatari sana katika safu yao ya ushambuliaji, Lionel Messi, Neymar na Suarez huku Iniesta akimiliki kasi ya mchezo katika eneo la kiungo," aliongeza
"Wamekuwa wakicheza fainali nyingi sana, lakini hatutakuwa na hofu juu ya hilo kwa sababu ya uzoefu na mtazamo wetu chanya ambao ni faida kubwa sana kwetu".
"Tutaangalia katika maeneo yote, ama kisaikolojia au kimwili ili tujiweke sawa katika mchezo wetu."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video