Na Mahamud Rajabu
Wawakilishi pekee wa michuano ya kimataifa timu ya Yanga SC, leo wameendeleza wimbi la ushindi na kuzidi kuukaribia ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara mara baada ya kuwatungua wanajeshi wa Ruvu Shooting kwa jumla ya mabao 5-0, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Dalili za Yanga kuibuka na ushindi zilianza kuonekana mapema kabisa baada ya kuanza mpira kwa kasi na kulisakama lango la Ruvu Shooting huku Msuva akikosa bao la wazi mnamo dakika ya nne tu ya mchezo.
Yanga waliandika bao lao la kwanza mnamo dakika ya 13 kupitia kwa Simon Msuva baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliyochongwa kwa umahiri wa hali ya juu na Haruna Niyonzima 'Fabregas'.
kutokana na kufungwa goli hilo, Ruvu Shooting nao walijibu shambulizi langoni mwa Yanga dakika ya 14 lakini hata hivyo shuti la Yahya Tumbo lilitoka nje.
Yanga nao walifanya Shambulizi lingine langoni mwa Ruvu Shooting dakika ya 21 lakini shuti la Oscar Joshua likidakwa na mlinda mlango Abdallah Rashid.
Alikuwa ni Kpah Sherman ambaye aliifungia Yanga bao la pili mnamo dakika ya 24 baada ya kuunganisha mpira wa kona uliochongwa na Haruna Niyonzima.
Wakihangaika ili walau nao wapate goli, Ruvu Shootings walifanya shambulizi lingine tena langoni mwa Yanga mnamo dakika ya 31 lakini Abdulrahman Musa alikosa nafasi hiyo.
Ilikuwa ni almanusura Msuva aiandikie Yanga bao la tatu baada ya kuachia shuti kali kabisa langoni mwa Ruvu Shooting na kugonga mwamba.
Msuva alipiga shuti kali kwa mara nyingine tena lakini lilitoka lilipaa juu kwa umbali mdogo sana
Yanga walipata bao la tatu kupitia kwa Msuva tena mnamo dakika ya 45 baada ya kuunganisha mpira kwa kichwa maridadi kabisa kutokana na krosi iliyochongwa na Hruna Niyonzima.
Yanga walizidi kuliandama lango la wanajeshi hao kutoka mkoani pwani baada ya Mrisho Khalfani Ngassa kuachia shuti kali dakika ya 50 na kugonga mtambaa wa panya na kutoka nje.
Ruvu Shooting siku ya leo walionekana kutepeta kabisa mbele ya Yanga mara baada ya kujikuta wakifungwa goli la nne lililowekwa kimiani na Amissi Jocelyn Tambwe kutokana na pasi nzuri iliyopigwa na Haruna Niyonzima.
Yanga walizidi kupeleka msiba kwa Ruvu Shooting ambapo Kpah Sherman ambapo hapo awali alikuwa akiandamwa na mzimu wa ukame wa mabao kwa mara nyingine tena alitumbukiza kimiani mpira kwa kichwa baada ya kupokea krosi iliyochongwa kwa uzuri na Juma Abdul kutoka upande wa kulia mwa uwanja.
Wakinekana kujikongoja ili walau wapate goli la kufutia machozi, Ruvu Shooting walifanya shambulizi langoni mwa Yanga dakika ya 75 na 83 lakini hata hivyo juhudi zao hazikuzaa matunda.
Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kutoa kipigo kama hiki kwa Ruvu Shooting mara baada ta kufanya hivyo msimu uliopita kwa kuwatungua mabao saba kwa bila, mchezo ambao pia ulipigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Ruvu Shooting walipata kona mbili wakati Yanga walipata kona tano.
Mwamuzi Isihaka Shirikisho aliwazawadia kadi za njano wachezaji Kelvin Yondani na Andrey Coutinho kwa upande wa Yanga na George Osei na Yahya Tumbo kwa upande wa Ruvu Shooting.
Yanga walipata kona tano huku Ruvu Shooting wao walipata kona mbili tu katika kipindi chote cha mchezo.
Ruvu Shooting:Abdallah Rashid, Michael Aidan, Abdul Mpambika, George Osei, Hamis Seleman, Salvatory Ntebe, Raphael Kyala, Ally Khan, Yahya Tumbo, Bakari Mtuwi/Juma Mpakala (49), Abdulrahman Musa; Subs: Bidii Hussein, Said Madega, Adam Seseme, Mwita John, Juma Nade, Hamis Saleh;
Kocha: Tom Olaba
Yanga: Ally Mustapha, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondan, Said Juma/Andrey Coutinho, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa, Kpah Sherman/ Hussein Javu; Subs: Deogratius Munishi'Dida', Andrey Coutinho, Pato Ngonyani, Danny Mrwanda, Hassan Dilunga na Edward Charles:
Kocha: Hans Van Der Pluijm.
Mwamuzi;
Isihaka Shirikisho.

0 comments:
Post a Comment