UONGOZI
wa Yanga umewakaribisha wananchi wote kujitokeza leo uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam kusherekea ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania.
Yanga inakabiliana
na Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu itakayoamua ubingwa kwasababu
wanahitaji pointi tatu tu kutawazwa mabingwa wapya.
Mpaka
sasa Yanga wanaongoza katika msimamo wa ligi kuu kwa pointi 52 na kama
watashinda leo watafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Mkuu wa
Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ameuambia mtandao huu kuwa
uongozi umeandaa ‘staili’ ya aina yake kushangilia ubingwa leo.
“Kama
una wasiwasi kuwa Yanga hawawezi kuwa mabingwa leo basi una matatizo, kama
kawaida yetu leo tunabeba kombe kwa kumpiga mtu (Polisi Moro) goli nyingi”.
Amesema Muro na kuongeza: “Hakuna wa kutuzuia, wananchi waje kwa wingi
kushangilia ubingwa wetu wa mapema”.
0 comments:
Post a Comment