Hawa ni wachanga?
AFISA
habari wa Simba, Hajji Sunday Manara amepingwa kwa kauli yake anayotoa kuwa
Simba ni timu changa hususani inapofungwa katika mechi za ligi kuu soka
Tanzania bara.
Simba imefungwa
mechi tano katika mechi 23 walizocheza mpaka sasa. Walianza kufungwa goli 1-0
dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Taifa, wakafungwa 2-1 dhidi ya Mbeya City
uwanja wa Taifa, wakafungwa 1-0 na Stand United uwanja wa Kambarage, wakapoteza
2-0 dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani na juma lililopita walichapwa 2-0
na Mbeya City uwanja wa Sokoine.
Hajji Sunday Manara (kushoto), msemaji wa Simba SC
Mwanachama
wa Simba, Ahmed Rashid Msahaba alipohojiwa na E fm jana alisema kauli ya Hajji
kwamba ni Simba ni timu changa ni porojo tu na yeye anaikaa.
“Msemaji
wetu Hajji Manara ni kijana wetu ambaye tunampenda, ni mwanachama mzuri, lakini
kauli yake kwamba Simba tunafungwa eti kwasababu wachezaji wetu bado ni
wachanga mimi nakataa’, Alisema Msabaha na kuongeza, “Tunaposhinda anakwambia
timu yetu nzuri, tunapofungwa anasema timu changa, hivi ukichukua wachezaji wa
Mbeya City, Ndanda, Stand United inatofautiana uwezo na Simba kweli? Simba ina
uwezo kuliko timu zote hizo, hao wachezaji wa Simba wamechaguliwa mpaka timu ya
taifa. Anaongea Porojo, timu ina wachezaji kutoka Uganda, anasema Simba haina
uwezo, wao wameshindwa kuongoza timu kama tulivyotarajia”
“Tatizo
lipo kwenye uongozi wa klabu ya Simba, wameshindwa, tumewachagua viongozi wale lakini
uwezo wao ni mdogo, angalau wangechagua
kamati ambazo zingewasaidia kuliko kuchagua kamati kwa urafiki, kwasababu tu
waliwapigia debe”.
Ukiangalia
kiuhalisia, Simba ina wachezaji ambao hawajakaa pamoja kwa muda mrefu mfano,
Danny Sserunkuma, Simon Sserunkuma, Juuko Mursheed ni Waganda waliosajiliwa kwa
wakati mmoja, labda Emmanuel Okwi na Joseph Owino angalau wana wana uzoefu
zaidi ya waganda wenzao.
Hata
wachezaji wazawa wengi ni vijana wadogo ambapo wapo kwenye umri wa kuendelea
kujifunza soka, hivyo ni rahisi kuwa na makosa ya hapa na pale. Mfano akina Manyika
Peter, Said Ndema, Mohamed Hussein, Hassan Kessy, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib.
Bahati
mbaya zaidi Simba imekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha, hii
imeleta athari ya moja kwa moja kwa vijana hawa.
Ukiangalia
Yanga, Azam zina wachezaji waliokaa pamoja kwa muda mrefu kuliko Simba. Pia
hawajabadili sana makocha ndani ya miaka mitatu iliyopita.
Angalia
Simba kutoka Milovan Circovic wa mwaka 2012 wanachukua Ubingwa mpaka sasa
wamepita mikononi mwa Patric Liewig, Abdallah Kibadeni, Zdravko Logarusic,
Patrick Phiri na sasa Goran Kopunovic.
Lakini ukweli
ni kwamba hata uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva hauko sawa hasa kwa
kuendeleza migogoro inayoigawa timu wakati kauli yao inasema Simba Nguvu Moja.
0 comments:
Post a Comment