Mshambuliaji wa Man United Robin van Persie, ameonesha dalili zote kwa kocha wake Louis van Gaal kuwa bado anahitaji kubaki klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika.
Van Persie ambaye msimu huu ameitumikia klabu hiyo mara chache kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara, amecheza mechi 25 huku akifunga magoli 10 tu katika michuano yote.
Lakini hata hivyo Van Persie mwenye ambaye atakuwa anatimiza miaka 32 kabla ya msimu ujao kuanza anasemekana kuyafurahia maisha ya klabuni hapo na yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment