Saturday, April 25, 2015

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal anaamini kwamba klabu hiyo itamuajiri Ryan Giggs kama mrithi wake.
Giggs mwenye umri wa miaka 41 alisimamia mechi nne msimu uliopita baada ya aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes kupigwa kalamu,kabla ya yeye kupewa kazi ya kuwa msaidizi wa Van Gaal.
Van Gaal ambaye atafikisha miaka 63 anakamilisha msimu wake wa kwanza kama kocha wa Man United na kandarasi yake inamalizika mwaka 2017.
Alipoulizwa kuhusu Giggs,kocha huyo aliiambia runinga ya klabu hiyo kwamba anatumai kwamba ndiye atakayemrithi.
"Natumaini kwamba ndiye atakayechukua mikoba yangu baada ya mimi kuondoka hapa," Van Gaal aliiambia runinga ya Man United.
"Lakini sasa mimi ndiye ninayewajibika. Yeye anafanya vitu kama ambavyo wanafanya wachezaji kwa sasa, na mara nyingi ninachomwambia afanye huwa anafanya, tena kwa ustadi wa hali ya juu.
Giggs alisema kwamba alifurahi sana alipopewa jukumu la kuisimamia kilabu hiyo baada ya Moyes kupigwa kalamu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video