Mark Vivian Foe alianguka uwanjani ikiwa ni dakika ya 72 kwenye mechi ya Fifa Confederation cup na kutokana na ugonjwa wa moyo na kupelekea kupoteza maisha. Hadi leo namba alizowai kuzivaa Foe kwenye club za Manchester city na kwingine zimekua retired kwa heshima yake.
Tukio kama hilo lilibakia kidogo tu litokee kwenye mechi ya soka huko ubeligiji ambacho mchezaji Gregory Mertens alianguka akiwa mchezoni kutokana na ugonjwa wa moyo (Cardiac Arrest). Beki wa huyo wa timu ya Lokeren mwenye miaka 24 akiwa kwenye mechi dhidi ya Genk alianguka dakika ya 25.
Madktari wa timu walikimbia uwanjani kumpa huduma ya kwanza lakini ilibidi ambulance lije uwanjani kumbemba. Kutokana na afya ya mchezaji huyo ilibidi awe amepitia vipimo kadhaa lakini document za hivyo vipimo havikupatikana. Maana yake ni kwamba hakupata hivyo vipimo kabla kinyume na sharia na taratibu za mpira huko ulaya. Hivi sasa yupo hospitali anaendelea na matibabu.
0 comments:
Post a Comment