Friday, April 24, 2015

Shirikisho la soka Ulaya UEFA limemfungulia mashtaka kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola kwa kosa la kuvaa fulani ambayo ilikuwa na ujumbe ambao ulionekana kuvunja sheria za shirikisho hilo.
Kocha huyo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi ya marudiano dhidi ya Porto alivaa fulana iliyoandika "Justiciaparatopo" ambao ni ujumbe unachochea kampeni ya kutaka uchunguzi wa kifo cha mwandishi wa habari  Jorge Lopez ufanyike.
Mwandishi huyo wa habari za michezo wa Argentina alifariki julai mwaka jana  katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil baada ya teksi aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambalo lilikuwa limeibwa wakati likikimbizwa na polisi.
Shirikisho hilo limesema kuwa litatoa adhabu hiyo kwa kocha huyo baada ya kukiuka sheria za kimichezo. "Mimi niliamka asubuhi, familia ilinipa fulana ,hivyo nikavaa,sioni kama kuna kosa lolote " alisema Guardiola.
Kikosi cha kocha huyo kimefuzu hatua ya nusu fainali katika michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuitoa FC Porto kwa jumla ya goli 7 kwa 4 katika hatua ya robo fainali siku ya jumanne ya wiki hii.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video