BODI ya ligi kuu soka Tanzania bara (TPLB) kupitia kwa
mwenyekiti wakati Ahmed Yahya bado haijapanga siku rasmi ya kuwakabidhi Yanga
ubingwa wao na zawadi nyingine.
Yahya amesema siku ya kuwakabidhi ubingwa ni baada ya ligi
kuu kumalizika na hawezi kuwakabidhi wakati ligi bado haijamalizika.
“Siku (ya kukabidhi ubingwa) haijapangwa bado kwasababu ligi
haijamalizika, ligi ikimalizika tutapanga siku ya kutoa zawadi na kuwakabidhi
ubingwa wao rasmi, lakini wana haki ya kushangilia. Nitumie nafasi hii
kuwapongeza Yanga kwa kuibuka mabingwa wa Tanzania bara”.
“Hatuwezi kuwakabidhi ubingwa mapema kwasababu tunafuata
sheria na kanuni zetu, tutawakabidhi baada ya kumalizika kwa mashindano,
hatuwezi kuwakabidhi hapa katikati, ni mabingwa kwa matokeo, lakini ligi bado
haijaisha, ligi inamalizika tarehe 9 mwezi wa tano, hapo tutakuwa na nafasi
kuwakabidhi ubingwa na zawadi nyingine zikafuata baadaye kidogo”.
Mchana wa leo shirikisho la soka Tanzania bara, TFF, kupitia
kwa afisa habari wake, Baraka Kizuguto lilituma taarifa kwa vyombo vya habari
likieleza kuwa Yanga watakabidhiwa ubingwa aprili 6 mwaka huu kwenye mechi ya
ligi kuu baina ya Azam fc na Yanga.
Lakini kauli ya mwenyekiti wa bodi inaonesha kutofautiana na
TFF.
Taarifa iliyotumwa mchana kwa vyombo vya habari na Baraga
Kiziguto hii hapa:
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa
Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu zake za
pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa
wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika
mwakani.
Klabu ya Young
Africans imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 (ishirini na tano)
jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro
katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya ligi
kumalizika.
Waziri
wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dr. Fennela Mkangara anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Mei 6, 2015 katika mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Young Africans.
0 comments:
Post a Comment