MFALME wa taarabu nchini, Mzee Yusuph ambaye ni shabiki wa
Yanga amesema haya baada ya timu hiyo yenye masikani yake mitaa ya Twiga na
Jangwani kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu 2014/2015.
Yanga iliifunga Polisi Morogoro 4-1 jana uwanja wa Taifa na
kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
“Dirisha la kwanza nadhani kocha (Marcio Maximo) alishindwa,
wachezaji walimshinda. Dirisha la pili wachezaji wamefanana na kocha, kocha anajua nini anafanya,
kukosa ubingwa haukuwa kitu rahisi, yaani Yanga kukosa ubingwa kwa timu
waliyokuwa nayo, haiwezekania”.
“Mapema watu walishamaliza shughuli yaani kama ubwabwa
ushaliwa, walishachelewa jamvini, nazungumza na maswahiba zetu, walishachelewa
jamvini, karamu tayari ishamalizika, wasubiri makombo tena”
Mzee Yusuph pia amezungumzia Kuhusu mechi ya marudiano ya
kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora baina ya Etoile du Sahel na Yanga
itayopigwa mwishoni mwa juma hili nchini Tunisia.
Mechi ya kwanza uwanja wa Taifa, timu hizo zilitoka sare ya
1-1.
“Tatizo walipokuja hapa (Etoile) kuna wachezaji hawakufanya
kazi yao vizuri, nadhani kocha hakuliona haraka. Kama ameshaliona tatizo
sidhani kama litatokea, Yanga wana uwezo wa kuwafunga, japo Yanga watafungwa
lakini wana uwezo wa kurudisha tena, chochote kinaweza kutokea, sizungumzi
mpira duara, wale jamaa wanajua, wapo kwenye ‘Levo’ ya kujua nini wanafanya,
miundombinu yao, wanajua kucheza na mambo ya nje ya uwanja, lakini lolote
linaweza kutokea, sidhani kama Yanga watamiminiwa mvua ya magoli kama
tulivyotegemea, Yanga wakibadilisha
tatizo la katikati lililokuwepo kipindi kile, kocha akiliona hili, tutafanya
vizuri”
“Nawaambia mashabiki waendelea kuisapoti timu kwasababu bila
umoja hakuna umoja, sio kwenda mbele tu, unaenda mbele peke yako, Daima mbele
nyuma mwiko maana yake muende mbele wote. Matatizo madogo madogo yanatokea, timu kama hii kufungwa na Simba ni aibu”
0 comments:
Post a Comment